Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Wahid Khorasani katika tamko lake alisema kuwa Utumishi ulio mkubwa zaidi siku hizi ni kuhuisha masiku ya Fatwimiyya, na akaongeza kuwa: “Jambo la Bibi Zahra (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) lina upekee kwa kuwa linajumuisha nguzo mbili: Tawalli na Tabarri.”
الْأَصْبَغُ بْنُ نُبَاتَةَ أَنَّهُ سَأَلَ [سُئِلَ] أَمِیرَ الْمُؤْمِنِینَ عَنْ [عِلَّةِ] دَفْنِهَا لَیْلًا؟ فَقَالَ: إِنَّهَا کَانَتْ سَاخِطَةً عَلَی قَوْمٍ کَرِهَتْ حُضُورَهُمْ جِنَازَتَهَا وَ حَرَامٌ عَلَی مَنْ یَتَوَلَّاهُمْ أَنْ یُصَلِّیَ عَلَی أَحَدٍ مِنْ وُلْدِهَا»Asbagh bin Nubata anasema: Watu waliuliza kuhusu Amiri al-Mu’minin (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) kuhusu sababu ya Bibi Fatima kuzikwa usiku. Akasema: “Kwa sababu Fatimah al-Zahra alikuwa amewakasirikia watu fulani, na hakuridhia wao kuhudhuria mazishi yake. Na kwa wale wanaowapenda watu hao, ni haramu kuswali juu ya jeneza la yeyote miongoni mwa watoto wa Bibi Fatima.” (1)
Ni kitu gani kilitokea mpaka Faatimah al-Zahra akaghadhibika?
Ni kitu gani kilitokea mpaka akatangaza kwamba haridhii wahudhurie kwenye mazishi yake?..
Al-Amali, Sheikh al-Saduq, uk. 755;
Imenukuliwa kutoka katika kauli za Ayatullah Wahid Khorasani.
Maoni yako